Akisoma tamko la kanisa hilo jijini Dar es Salaam jana, kwa niaba ya viongozi wa Jimbo, Katibu Mkuu wa Jimbo la Misheni Mashariki, Emmaus Mwamukula, alisema kanisa hilo linasitisha mahusiano na jimbo hilo.
Alisema Kanisa hilo linatambua kuwepo kwa Wakristo na shirika zinazopingwa vitendo hivyo ndani ya Jimbo la Amerika ya Kaskazini na kwamba Jimbo hilo litakuwa kushirikiana na wakristo hao pamoja na shirika zao.
Katibu huyo alisema halmashauri Kuu imebaini kuwa Mwenyekiti wa Kanisa la kanisa hilo jimbo la Amerika ya Kaskazini, hivi karibuni amekuwa na ukaribu na baadhi ya viongozi wanaounga mkono upande mmoja wa mgogoro uliopo Jimbo la Misheni ya Mashariki.
“Ukaribu huo unawatia nguvu viongozi wanaovamia shirika na kuleta fujo makanisani, kwa kuwa Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Jimbo la Amerika ya Kaskazini pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Kanisa hilo duniani, nafasi yake imetumika sana kuwapa nguvu kundi moja Jimboni kwetu,” alisema.
Alisema mamlaka ya mwisho kuhusiana na masuala ya imani ya Kikristo ni neno la Mungu ambalo ni Biblia, ambayo inatamka wazi kuwa vitendo vya ushoga na usagaji ni chukizo mbele za Mungu na kwamba watendao marendo ya namna hiyo hawataurithi ufalume wa Mungu.
Mwamakula alisema kutokana na hali hiyo kundi hilo limeendelea kufanya fujo katika shirika mbalimbali kama Kinondoni, Malinyi, Ruaha Mahenge, Kimara, Boko (Sayuni) na Tabata.
Aidha, kanisa hilo linatoa wito kwa wakristo wa Mashariki kukataa kwa namna zote ushoga na usagaji ikiwa ni pamoja na kuwakataa viongozi wanaoshikamana na watu waliohalalisha ushoga katika majimbo yao na kwamba majimbo mengine yanayopinga yaunge mkono kwa kutoa tamko.
Alisema kanisa hilo litaendelea kuwaombea viongozi wa Kanisa la Moraviano Jimbo la Amerika ya Kaskazini ili wafikie hatua ya kufikiria toba. CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment