BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SH1.5/- TRILIONI ZAHITAJIKA KUINUSURU RELI YA KATI.

Kiberenge kikipita kwenye daraja la reli ya kati la Mzaganza ambalo ujenzi wake umekamilika. Daraja hilo lililoko Kilosa mkoani Morogoro lililosombwa na maji baada ya mvua kubwa zilizonyesha mwaka 2010. Ukarabati wake uligharimu Sh11.1 bilioni. Picha na Juma Mtanda.

Na Juma Mtanda, Mwananchi

Morogoro. Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahaco), imesema kiasi cha Sh1.5 trilioni kinahitajika kukarabati reli ya kati ili iweze kurudi katika hali yake ya kawaida.



Hayo yalisemwa juzi na mhandisi mwandamizi wa miradi wa Rahaco, Maizo Mgedzi alipokuwa akitoa taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Kamati hiyo ilikuwa wilayani Kilosa kukagua reli ya kati ambayo mara nyingi katika kipindi cha mvua, imekuwa ikiharibikla kutokana na mafuriko.


Mgedzi alisema kama Shirika la Reli litatengewa Sh500 bilioni kila mwaka, litaweza kuimarisha reli hiyo na hivyo kutoa huduma bila kusuasua.


Alisema bajeti ndogo imekuwa kikwazo katika jitihada zake za kuboresha reli na huduma nyingine inazopaswa kuzitoa.


Mhandisi huyo alitoa mfano wa mwaka wa fedha ulioisha kwamba shirika hilo liliomba Sh174 bilioni, likapewa Sh29 bilioni.


Kwa upande wake, mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe alisema ataiomba Serikali katika bajeti ya 2015/2016, itenge fedha zaidi kwa shirika hilo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: