TFF YAVUNA FEDHA ZA UTOVU WA NIDHAMU BAADA YA KUTOA ADHABU LIGI KUU TANZANIA BARA.
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia mechi tatu beki George Michael Osei wa Ruvu Shooting kutokana na makosa ya kinidhamu aliyoyafanya akiwa uwanjani.
Osei ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumkaba na kumchezea kibabe mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe ambapo ni kinyume na mchezo wa kiungwana (fair play) ameadhibiwa kwa kuzingatia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Mlalamikiwa alifika mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema Osei alipopewa nafasi ya kujitetea alikana kufanya kosa hilo na kudai magazeti yametengeneza picha hizo. TFF iliwasilisha ushahidi wa magazeti mawili ya Championi na moja la The Guardian kwa kuzingatia Ibara ya 96(3) ya Kanuni ya Nidhamu ya TFF Toleo la 2012.
Katika uamuzi wake, Kamati imesema kitendo cha Osei ni kinyume na kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair play), na kuongeza kuwa kanuni za TFF kwa makosa kama hayo ni dhaifu, hivyo kuagiza zirekebishwe ili ziweze kuwa kali zaidi.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo, imetupa malalamiko yaliyowasilishwa na TFF dhidi Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Mugisha Galibona, na Katibu wa Simiyu (SIFA), Emmanuel Sorogo.
Kwa upande wa Sorogo, Kamati imesema baada ya kupitia vielelezo vya pande zote, hasa upande mlalamikiwa imeridhika kuwa hakushiriki katika kumpiga refa kwenye mechi ya Kombe la Taifa kwa Wanawake kati ya Shinyanga na Simiyu.
Badala yake aliyehusika ni Kocha wa Simiyu, Emmanuel Babu ambaye tayari uongozi umeshachukua hatua dhidi yake kwa kumsimamisha kwanza wakati akisubiri kufikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya SIFA.
Pia barua ya kumsimamisha kocha huyo ilitumwa kwa Katibu Mkuu wa TFF na Mkurugenzi wa Mashindano. Kamati imeyachukulia maneno ya mlalamikiwa kuwa ni sahihi ndiyo maana hayakupingwa na TFF, hivyo malalamiko dhidi ya mlalamikiwa hayana msingi na yametupwa.
Kwa upande wa Galibona ambaye ripoti za Kamishna na refa zilionyesha kuwa alishiriki kuhamasisha marefa kupigwa baada ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Polisi Mara FC na Mwadui FC, Kamati imesema mlalamikiwa aliwasilisha vielelezo vinne kuthibitisha kuwa hakuhusika.
Kamati imesema licha ya ripoti ya Saleh Mang'ola kumtaja Galibona, lakini maelezo ya refa huyo na msaidizi wake Rebecca Mulokozi waliyoandika Kituo cha Polisi baada ya tukio hilo hayakumtaja mlalamikiwa mahali popote.
Pia barua ya FAM kwenda TFF kuhusu matukio ya mechi hiyo yanamtoa hatiani mlalamikiwa, hivyo Kamati imeamuru kuwa malalamiko dhidi ya Galibona hayana msingi na yametupiliwa mbali.
KIONGOZI VILLA SQUAD APIGWA FAINI 600,000/-
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa Squad, Mbarouk Kassanda kwa kusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao haukufuata kanuni za usajili.
Villa Squad iliingiza majina tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala ya Omari Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim'. Kamati imeona Villa Squad ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa kielektroniki ukubali jina la mchezaji.
Malalamiko ya kutaka kupewa pointi tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad kwa kumchezesha mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni mchezaji halali aliyethibitishwa (eligible) na TFF.
Kamati ilimuita mchezaji huyo na kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa kubadili majina ili aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili lilibaki kuwa suala la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati haikupata ushahidi thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida ya mashaka (benefit of doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.
Kassanda ameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) wakati Omari Ramadhan ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu hiyo.
JKT MLALE YATAKIWA KUILIPA LYON
Klabu ya JKT Mlale imeamriwa kuilipa African Lyon jumla ya sh. 600,000 ikiwa ni ada ya uhamisho na fidia kwa kumtumia mchezaji Noel Lucas kinyume cha taratibu kwenye mechi.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya kusikiliza malalamiko ya African Lyon ambapo ilibaini kuwa klabu hiyo ilikubali kulipwa sh. 300,000 ilikwa ni ada ya uhamisho.
Kamati imekataa maombi ya African Lyon kutaka pointi tatu na mabao matatu katika mechi yao ambapo Noel Lucas alicheza, kwa vile mchezaji huyo usajili huo ulithibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Pia JKT Mlale imetakiwa kuilipa African Lyon sh. 300,000 nyingine za usumbufu wa kufuatilia malipo ya mchezaji huyo. JKT Mlale imetakiwa kulipa fedha hizo kabla ya mechi yake ya mwisho ya ligi.
JUDICIAL AND STANDING COMMITTEES.
Kamati ya Utendaji iliyoketi tarehe 19 Disemba 2014, ilifanya mabadiliko katika kamati ndogo ndogo na zile za kisheria. Kamati hizo ni kama ifuatavyo
KAMATI YA NIDHAMU
1. Tarimba Abbas (Mwenyekiti)
2. Advocate Jerome Msemwa ( Makamu mwenyekiti)
3. Kassim Dau
4. Nassoro Duduma
5. Kitwana Manara.
KAMATI YA RUFANI YA NIDHAMU
1. Advocate Mukirya Nyanduga (Mwenyekiti)
2. Advocate Revocatus Kuuli (Makamu mwenyekiti)
3. Abdala Mkumbura
4. Dr. Franics Michael
5. Advocate Twaha Mtengela
KAMATI YA MAADILI
1. Advocate Wilson Ogunde (Mwenyekiti)
2. Advocate Juma Nassoro (Makamu mwenyekiti)
3. Advocate Ebenezer Mshana
4. Geroge Rupia
5. Mh. Said Mtanda
KAMATI YA RUFANI YA MAADILI
1. Advocate Walter Chipeta (Mwenyekiti)
2. Magistrate George Kisagenta (Makamu mwenyekiti)
3. Lilian Kitomari
4. Advocate Abdala Gonzi
KAMATI YA UCHAGUZI
1. Advocate Melchesedeck Lutema
2. Advocate Adamu Mambi (Makamu mwenyekiti)
3. Hamidu Mahmoud Omar
4. Jeremiah John Wambura
5. John Jembele
KAMATI YA RUFANI TA UCHAGUZI
1. Advocate Julius Lugaziya (Mwneyekiti)
2. Advocate Machare Suguta (Makamu Mwenyekiti)
3. Idrisa Nassor
4. Paschal Kihanga
5. Benister Lugora
KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO
1. Wallace Karia (Mwenyekiti)
2. Yahya Mohamed (Makamu mwenyekiti)
3. Goodluck Moshi
4. Omar Walii
5. Ellie Mbise
6. Deo Lubuva
KAMATI YA MASHINDANO
1. Geofrey Nyange (Mwenyekiti)
2. Ahmed Mgoyi (Makamu mwenyekiti)
3. James Mhagama
4. Stewart Masima
5. Steven Njowoka
6. Said Mohamed
KAMATI YA UFUNDI
1. Kidao Wilfred (Mwenyekiti)
2. Athumani Kambi (Makamu mwenyekiti)
3. Vedastus Rufano
4. Dan Korosso
5. Pelegriunius Rutahyugwa
KAMATI YA MPIRA WA MIGUU YA VIJANA
1. Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti)
2. Khalid Abdallah (Makamu mwenyekiti)
3. Ali Mayay
4. Mulamu Ngh’ambi
5. Said Tully
KAMATI YA MPIRA WA MIGUU WANAWAKE
1. Blassy Kiondo (Mwenyekiti)
2. Rose Kissiwa (Makamu mwenyekiti)
3. Zena Chande
4. Amina Karuma
5. Zafarani Damoder
6. Beatrice Mgaya
7. Sofia Tigalyoma
8. Ingrid Kimario (Katibu wa Kamati)
KAMATI YA WAAMUZI
1. Saloum Umande Chama (Mwenyekiti)
2. Nassoro Said (Makamu mwenyekiti)
3. Charles Ndagala (Katibu)
4. Kanali Issaro Chacha
5. Soud Abdi
KAMATI YA HABARI NA MASOKO
1. Athuman Kambi (Mwenyekiti)
2. Alms Kasongo (Makamu Mwenyekiti)
3. Rose Mwakitangwe
4. Amir Mhando
5. Haroub Selemani
KAMATI YA UKAGUZI WA FEDHA
1. Ramdhan Nassib (Mwenyekiti)
2. Epaphra Swai (Makamu mwenyekiti)
3. Jackson Songora
4. Golden Sanga
5. Francis Ndulane
6. Cyprian Kwiyava
KAMATI YA TIBA
1. Dr. Paul Marealle (Mwenyekiti)
2. Dr. Fred Limbanga (Makamu mwenyekiti)
3. Dr. Mwanandi Mwankewa
4. Dr. Eliezer Ndelema
5. Asha Mecky Sadik
KAMATI YA FUTSAL NA BEACH SOCCER
1. Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti)
2. Hussein Mwamba (Makamu mwenyekiti)
3. Samson Kaliro
4. Shaffih Dauda
5. Boniface Pawassa
6. Apollo Kayugi
PRESIDENTIAL COMMISSION FOR AFFAIRS
1. Omar Abdulkadir (Mwenyekiti)
2. Emmanuel Chaula (Makamu mwenyekiti)
3. Victor Mwandiki
4. Riziki Majala
5. Zahra Mohamed
6. David Nyandu
PRESIDENTIAL COMMISSION ON BUSINESS AND INVESTMENTS
1. William Erio (Mwenyekiti)
2. Mbaraka Igangula
3. Advocate Iman Madega
4. Lt. Col Charles Mbuge
5. Philemon Ntalihaja
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment