BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

USHAHIDI WA VIDEO WATUMIKA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MOROGORO KESI YA SHEIKHE PONDA ISSA PONDA.

Mke wa Sheikhe Ponda Issa Ponda, Khadija Ahmad akisalimiana na mume wake muda mfupi kabla ya kuanza kusikiliza kesi yake inayomkabiri katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro leo mkoani Morogoro.
Juma Mtanda.
 
Shahidi wa saba katika kesi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, Mkuu wa Kitengo cha Utambuzi, Polisi Morogoro, Inspekta Jafert Msongole, jana alitoa ushahidi wake mbele ya Mahakama ya Mkoa wa Morogoro akieleza jinsi ilivyokuwa lazima Sheikh Ponda kurekodiwa kwa siri kwenye mkanda wa video.


Akiongozwa na Wakili Mkuu Mwandamizi wa Serikali, Bernard Kongola mbele ya Hakimu Mary Moyo, shahidi huyo alieleza jinsi mshitakiwa alivyotoa maneno ya uchochezi katika Kongamano la Eid Pili, Agosti 10, 2013 kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Morogoro.


Alidai kuwa Agosti 10, 2013 saa kumi na moja jioni, alimtuma askari wake mmoja kwenda kupiga picha za video katika kongamano hilo kwa kutumia kamera ndogo, ambayo haikuwa rahisi kugundulika.


Alidai kuwa video hiyo ilikuwa na matamshi ya uchochezi na uvunjifu wa amani, hivyo kuamua kuihifadhi na baadaye kuipeleka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kitengo cha Uchunguzi wa Picha ili iwe kama kielelezo katika kesi hiyo.


Alisema kurekodi picha za matukio mbalimbali ni utaratibu wa kitengo hicho na kwamba alimtuma askari wake baada ya kupata taarifa kuwa Sheikh Ponda angehutubia siku hiyo.


Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili, Juma Nasoro ulimuuliza maswali shahidi huyo, likiwamo la kutaka kujua kama kuwapo kwa Sheikh Ponda katika kongamano hilo kungevuruga amani.


Wakili Nasoro alimuuliza shahidi huyo kwa nini video hiyo ilirekodiwa sehemu ndogo aliyozungumza Sheikh Ponda na siyo mkutano wote.


Pia alitaka kujua maneno ya Sheikh Ponda ambayo yalikuwa ya uvunjifu wa amani yaliyorekodiwa.


Wakili mwingine wa upande wa utetezi, Abubakari Salimu alimuuliza shahidi huyo kwa nini jana alichelewa kufika mahakamani kutoa ushahidi alipoitwa?


Akijibu maswali hayo, shahidi huyo alidai kuwapo kwa Sheikh Ponda kwenye kongamano hilo kungeweza kuvuruga amani, kwa vile hakutakiwa kuwapo.


Akijibu swali la pili, alisema video hiyo ilirekodiwa sehemu ndogo kutokana na askari aliyemtuma kuchelewa kufika eneo la tukio.


Alidai kuwa ilikuwa lazima Sheikh Ponda arekodiwe kwenye video huku akisisitiza kwamba matamshi aliyotoa yalikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani. Kuhusu kuchelewa, alisema alitakiwa kuwa mbali na eneo la Mahakama, hivyo hata alipotakiwa kuingia ndani hakupata taarifa mapema. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 16 mwaka huu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: