WANAJESHI WATIBUA MIPANGO YA SHAMBULIO LA KIGAIDI, BAADA YA KUWAFYATULIA RISASI WASHUKIWA WATATU NA DEREVA WAO.
Vikosi vya usalama nchini Somalia vinasema kuwa vimetibua jaribio la mlipuaji wa kujitoa muhanga dhidi ya mkutano wa wanasiasa katikati ya taifa hilo.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wamewaua watu watatu waliojihami kwa bunduki pamoja na dereva wa gari lililojaa vilipuzi.
Kundi la wapiganaji wa AL Shabaab limekiri kutekeleza uvamizi huo katika mji wa Adado.
Pia limesema kuwa lilishambulia vikosi vya Amisom pamoja na majeshi Somalia.
Al Shabaab limekuwa likiongeza mashambulizi yake wakati wa mwezi mtukufu wa Ramdhan ambao umeanza.BBC
0 comments:
Post a Comment