BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI ATAKIWA KUANZA NA UDHIIBITI WA MFUMO WA ULIPAJI KODI KWA WAFANYABIASHARA.


Rais Dk. John Maghufuli ametakiwa kudhibiti mfumo wa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo nchini ili kuviwezesha viwanda vya ndani kufanya vizuri katika soko la ushindani la ndani na nje.

Pia, wameshauri serikali yake isiingilie masuala ya viwanda na badala yake iyaachie mashirika binafsi kusimamia ili kuwapo na uwiano sawa kwa wafanyabiashara hao katika utozwaji wa kodi.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Johnson Minja, aliitaka serikali kudhibiti mfumo wa kodi ambao ni chanzo cha kudidimiza ukuaji wa uchumi kwa wafanyabiashara.

Alisema baadhi ya viongozi wa serikali wa ngazi za juu huchangia mwenendo mchafu wa mfumo huo kwa maslahi ya wachache huku wakiliumiza kundi kubwa la wafanyabaishara wa kati na wadogo.

Minja alisema ili serikali isiingie katika msigano baina yake na wafanyabiashara, inatakiwa kuweka wazi suala la ulipaji kodi.

“Ushauri wangu kwa Rais Dk. Magufuli, aangalie suala hili kwa makini ili kuwasaidia wafanyabaishara wakubwa, wa kati na wadogo kwa sababu kila mmoja anatakiwa kutozwa kodi kulingana na kiasi cha bidhaa zake,” alisema Minja.

Kwa upande wake, Mchumi wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Hussein Kamota, aliitaka serikali kuhakikisha bidhaa zinazoingia na kutoka nje zinatozwa kodi sahihi kulingana na kiwango cha bidhaa.

Alisema kutolewa kwa kodi halali kutatoa hamasa kwa wafanyabiashara hao kupanua wigo wa biashara ndani na nje wakati CTI ikijaribu kuzungumza na serikali kuhusu kupunguza baadhi ya kodi za bidhaa hizo.

Hata hivyo, CTI imewataka wanachama wake wote kujiepusha na uvunjifu wa kutotozwa kodi kwa sababu ikibaini hali hiyo, hatua stahiki zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.

“Ni muhimu kwa mmiliki wa kiwanda kama kulipa kodi, hivyo mwanachama lazima akubaliane na sheria za nchi, hivyo nasisitiza tutakapochunguza na kubaini hatua stahiki zitachukulliwa kwa mhusika,” alisema Kamota.

Naye mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza sabuni na dawa ya meno G$B Soap Industries Ltd cha Salasala Kunduchi jijini Dar es Salaam, Goodliving Makundi, alisema mkakati wa serikali wa kufufua viwanda vya ndani huenda hautazaa matunda kutokana na serikali hiyo kushindwa kudhibiti suala la kodi kwa wafanyabiashara wakubwa nchini. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: