
1. Hupigiwi simu hadi umpigie,
2. Hutumiwi sms hadi umtumie.
3. Usipomtafuta halalamiki wala hakuulizi.
4. Ukimpigia simu anakwambia yupo bize.
5. Ukimpigia simu usiku anakwambia anataka kulala au simu haina chaji, lakini ukikaa kidogo ukipiga tena unakuta inatumika.
Mwanaume au mwanamke mwenye tabia hizi hafai kuwa mpenzi wako mkimbie kama ukoma... Kwa hiyo mwaka 2016 uwe ni mwaka wenye malengo mitazamo mipya na kufanikisha utakayo hakikisha unajipenda kwanza mwenyewe kuliko akupendavyo mtu mwingine.
Fanya kazi kwa bidii kama uko shule soma kwa bidii ukiwa na malengo, Be smart, vaa upendeze nukia vizuri then enjoy your life.
Kumbuka kuwa wanaume au wanawake wapo wengi sana so asikupasue kichwa mtu kama huyo.
We bado mdogo mrembo mnno kama huamini nenda kwenye kiyoo jitizame kisha tabasam anza maisha mapya, kama ni mkaka lazima utakuwa mtanashati na mwenye malengo yupo aliezaliwa kwa ajili yako ipo siku mtakutana na utakuwa mwenye furaha tena.
Acha kabisa kujilazimisha kwa mtu asiekujali wala kukufikiria usiwe mtumwa wa mapenzi, hakuna kitabu kilichoandika kuwa utakufa usipokuwa na mpenzi....
Jifikirie wewe kwanza jipende wewe Nmtangulize muumba wako kwa kila ufanyalo na mengine yatafuata.
0 comments:
Post a Comment