Kutokana na hali hiyo, Minja alilazimika kufunga safari hadi kwa mkuu wa hifadhi hiyo ili kujua nini tatizo na kuangalia namna ya kuweza kutatua baina ya uongozi wa hifadhi na wafugaji, tukio hilo lilitokea mwisho mwa Desemba 2015.
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Morogoro, Devotha Minja wa kwanza kulia akifuatilia jambo.
Ukweli wa jambo hilo ilikuwa mifugo iliyokuwa ikishikiliwa na askari wa wanyamapori Mikumi walikuwa 172 kati ya mifugo hiyo ilikuwa ikinyonyesha, kutokana na kushikiliwa kwa zaidi ya siku nne baadhi ya ndama sita walifariki dunia kwa kukosa chakula kutoka kwa mama yao.
Baada ya mazungumzo marefu kati ya Mbunge huyo, wafugaji na uongozi wa Mikumi, wafugaji walilidhia kulipa faini ya Tsh10,000 kwa kila mfugo mmoja kama adhabu ya kwanza na kama mfugaji atarudia kosa hilo hilo adhabu inayofuata ni kupigwa faini ya Tsh20,000 na adhabu ya tatu ni Ths30,000 kwa kosa hilo hilo.
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Morogoro, Devotha Minja akisaini kitabu cha wageni
0 comments:
Post a Comment