Watu katika miji mbalimbali walijitokeza kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2016 kwa njia mbalimbali. Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za hali ilivyokuwa.
Australia ilikuwa moja ya nchi za kwanza kuingia mwaka 2016, fataki zinaonekana hapa juu ya jumba la Opera House na daraja la Harbour Bridge.
Nchini Misri, fataki zinaonekana zikilipuka karibu na Piramidi.
Jijini Berlin, fataki zilitawala anga kama inavyoonekana hapa juu ya Lango la Brandenburg mjini Berlin.
Mjini London, hivi ndivyo hali ilivyokuwa karibu na Big Ben. Maelfu ya watu walijitokeza kutazama fataki.

Mji wa Baghdad haukuachwa nyuma, na hapa fataki zinaonekana zikilipuka katika Bustani ya Zawra.

Mjini Singapore, mwaka mpya ulikaribishwa kwa fataki. Hapa ni Marina Bay.

Mjini Kuala Lumpur, nchini Malaysia fataki zinaonekana zikilipuka karibu na jengo mashuhuri ya Petronas Towers.

Mjini Taipeni, Taiwan, fataki zinaonekana kwenye jumba refu la Taipei 101.

Mjini Paris, watu walikusanyika Champs Elysees kutazama video ya Mwaka Mpya iliyoonyeshwa katika Arc de Triomphe.

Nchini India, mwanamume huyo alitumia nyanya, vitunguu na pilipili kuandika 2016.

Mjini Auckland, New Zealand fataki zililipuliwa katika jumba la Auckland Sky Tower, mkesha wa Mwaka Mpya

Hapa, mwanamume anaonekana akitembea karibu na mapambo yaliyoandika 2016 katika mji wa Kiev, nchini Ukraine. GDP ya taifa hilo ilishuka asilimia 9 mwaka 2015.

Mjini Brazil, baadhi waliamua kufika katika ufuko wa Copacabana mjini Rio de Janeiro kuukaribisha mwaka mpya.

Mjini Beijing watu wengi waikusanyika kwa hafla iliyokuwa Hekalu la Tai Miao karibu na Forbidden City mjini Beijing.

0 comments:
Post a Comment