BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AMWAPISHA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI JAJI MEJA JENERALI IKULU DAR ES SALAAM.

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU NA WASAIDIZI WAO.

Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira akiapishwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa (Katibu Mkuu) Wizara ya Mambo ya Ndani.
 

Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli kabla ya tukio hilo alilazimika kuuliza swali kwa Makatibu wakuu wa wizara mbalimbali na Manaibu Katibu wakuu kama wameelewa na kukubali kusaini Kiapo cha Maadili katika Utumishi wa Umma mara baada ya kusoma maelezo yaliyomo katika kiapo hicho.


Baada ya kuapisha aliwauliza kama wanakubaliana na masharti yaliyomo kwenye kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma na kama yupo ambaye hakuridhia masharti hayo alipewa fursa ya ufafanuzi kabla ya kusaini kiapo hicho.

Makatibu wakuu na manaibu wao hata hivyo wote walisaini katika kiapo hicho.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)

Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu Maliasili na Utalii kushoto wakila kiapo cha maadili ya utumishi Ikulu leo.

Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakila kiapo cha Maadili ya Utumishi mbele ya Rais Dk. John Pombe Magufuli Ikulu leo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwaongoza Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu kusoma kiapo cha Maadili ya Utumishi kabla ya kusaini kiapo hicho.

Manaibu Katibu wakuu na Makatibu Wakuu wakisaini Kiapo hicho mara baada ua kusoma, kuelewa masharti yaliyomo na kuyakubali.

Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akitoa neno mara baada ya Makatibu hao kusaini kiapo cha Maadili ya Utumishi Ikulu leo.

Baadhi ya Makatibu Wakuu wakisubiri kuapishwa.

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. Goerge Masaju huku Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyamnge akifurahia kabla ya kuanza kwa hafla ya kuawaapisha Makatibu Wakuu.

Rais Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya kumuapisha Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba ikulu leo.

Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mh. Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu wizara ya Sheria na Katiba.

Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mh. James Dotto (Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango).

Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini)

Rais Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya kumuapisha Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini)

Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini).
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Immaculate Peter Ngwale kuwa (Naibu Katibu Mkuu)Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu – Afya)

Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa (Katibu Mkuu – Afya)

Rais Dk John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Laurian Ndumbaro kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora.

Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

Rais Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Vitendea kazi Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira mara baada ya kumuapisha kuwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akipiga saluti wakati wimbo wa taifa ulipokuwa ukipigwa .

Kutoka kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa , Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mwanasheria mkuu wa Serikali Mh. George Masaju.

Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu tayari kwa kuwaapisha Makatibu Wakuu na Mnaibu Katibu Wakuu leo, Kulia ni Balozi Ombeni Sefue Katibu Mkuu Kiongozi.

Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu Katubu wakuu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: