HATARI ! MKURUGENZI MTENDAJI BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU AFUTWA KAZI.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako. Picha ya Maktaba
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amemfuta kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), George Nyatenga kwa utendaji usioridhisha.
Wengine waliositishiwa mikataba ni pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo Onesmo Laizer.
“Nasitisha mkataba wake (Nyatenga) mara moja na hamna haja ya kumwandikia notisi, apewe mshahara wa mwezi mmoja,” amesema Profesa Ndalichako.
Pamoja na usitishaji wa ajira za wakurugenzi hao, Waziri Ndalichako ameagiza kufanyika ukaguzi wa ndani kwa lengo la kuhakiki nyaraka zilizowasilishwa Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa.MWANANCHI DIGITAL
0 comments:
Post a Comment