Juma Mtanda, Morogoro
Dereva wa lori aina ya fuso ambaye jina lake bado halijatambuliwa amenusuriki kifo baada ya kutumbukia mtoni na gunia 160 za mchele kufuatia mfumo wa breki kushindwa kufanya kazi wakati akiingiza gari gari ndani ya kivuko cha MV Kilombero II majira ya saa 9 alasiri juzi upande wa wilaya ya Ulanga mkoani Morooro.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka Ifakara, Mkuu wa kivuko cha MV Kilombero II, Fadhil Haroub amedhibitisha kutoka kwa ajali hiyo na kueleza kuwa baada ya dereva kuona mfumo wa breki kushindwa kufanya kazi alijiokoa na kuachaa gari likitumbikia majini.
Haroub alisema kuwa ajali hiyo imetokea wakati dereva huyo akiingiza gari katika kivuko lakini kutokana na breki kushindwa kufanya kazi, gari hilo lilipitiliza moja kwa moja na kuingia mtoni.
“Ni kweli kuna ajali ya fuso kutumbukia majini baada ya kufeli mfumo wa breki kwani ilishindwa kusimama katika kivuko wakati kivuko kimesimama upande wa Ulanga na kupitiliza hadi maji lakini tunashukuru dereva aliwahi kujiokoa”.alisema Haroub.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa lori hilo lilikuwa limebeba mchele na limetumbukia majini baada ya breki kufeli.
“Ni kweli kuna ajali ya lori aina ya fusi ambalo lilibeba mchele limetumbukia majini na juhudi za kuliopoa zinafanywa kwani limeziba njia ya kivuko na katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa.”alisema Matei.
Kamanda Matei ametoa wito kwa madereva kuchukua tahadhari mapema ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa magari yao kabla kuanza safari kwani itasaidia kubaini matatizo na kurekebisha kabla ya kuanza safari.

0 comments:
Post a Comment