BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LIONEL MESSI ASTAAFU SOKA KISA KUKOSA UBINGWA WA COPA AMERIKA 2016 MBELE YA CHILE.


MCHEZAJI bora mara tano duniani mshambuliaji wa Argentina na pia mabingwa wa Hispania Barcelona, Lionel Messi ametangaza kustaafu soka la kimataifa kufuatia kukosa bao wakati wa mipigo ya penati kwenye mchezo wa fainali ya Copa Amerika kati ya Argentina na Chile ikiwa imeweka rekodi ya kushindwa fainali ya nne kubwa katika muda wa miaka tisa.

Katika fainali hiyo, Chile ilishinda kwa penati 4-2 katika mtanange huo uliochezwa kwa dakika 120 kufuatia kumalizika kwa sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. 


Lionel Messi (29) alieleza ulimwengu kuwa: "Haikuwa bahati yangu na imetosha sasa kuchezea timu ya taifa, nimefanya kila ninaloweza, inauma kutokuwa bingwa."

Akiichezea Barcelona Messi ameshinda mataji manane ya La Liga na manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini taji lake pekee kubwa la kimataifa ni Medali ya Dhahabu ya michezo ya Olimpiki mwaka 2008.
 
Argentina ilifungwa na Ujerumani 1-0 katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 kabla ya kupoteza kwa mikwaju ya penati fainali mbili za Copa Amerika dhidi ya Chile. Argentina pia ilipoteza fainali ya Copa Amerika dhidi ya Brazil mwaka 2007 Messi akiwemo katika kikosi cha Argentina.

"Nimejaribu fainali nne. Ni kitu nilichokihitaji zaidi, lakini sikukipata, hivyo nafikiri ni mwisho," alisema.

"Nafikiri hii ni bora kwa kila mmoja. Kwanza kabisa kwangu mwenyewe, na kisha kwa kila mmoja. Nafikiri kuna watu wengi wanataka niachie ngazi, ambao ni wazi hawaridhishwi, kama ambavyo haturidhishwi kufika fainali lakini tunashindwa kutwaa mataji. 


"Ni vigumu sana, lakini nimechukua uamuzi. Sasa sitajaribu tena na sitabadili uamuzi."

Messi amefunga magoli matano katika fainali za mwaka huu za Copa Amerika likiwemo goli maridadi la adhabu katika nusu fainali dhidi ya Marekani na kuweka rekodi ya kuifungia Argentina magoli 55

Kwa mara ya kwanza Messi aliitwa kwenye kikosi cha Argentina mwaka 2005, na amecheza mechi 113 za timu hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: