BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIONGOZI WA KLABU YA SIMBA SC NAMNA WANAVYOIBA FEDHA MALI YA KLABU KWA KIVULI CHA MGONGO WA UONGOZI


Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Rage.
MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Rage amempa siku saba Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe kuthibitisha kauli aliyoitoa ya kumtuhumu kuhamisha fedha za mauzo ya Mbwana Samatta na kuweka kwenye akaunti ya mkewe.



Akizungumza jana, Rage alisema kauli ya Hanspope haina ukweli na imejaa chuki.


"Sijawahi kufanya hivyo, hata mke wangu hana akaunti benki. Wasitafute sehemu ya kutokea. Wakae pamoja na kutatua jambo hili wakabili," alisema Rage.


Alisema ameongea na mwanasheria wake ili kulifanyia kazi kauli ya Hanspoppe na kuangalia uwezekano wa kumfikisha mahakamani.


"Kama ana uthibitisho, aupeleke Takukuru ili na mimi niunganishwe kwenye sakata hilo," alisema Rage.


Aidha, alisema hapendi kulizungumzia suala la kukamatwa viongozi wa Simba, akiwamo Rais Evans, Aveva liko mbele ya vyombo vya sheria kwa sasa.


"Kwa sasa, bado ni tuhuma tu...tuache vyombo vya sheria vifanye kazi yake na mwisho tutajua ukweli wa jambo hili," alisema.


Alisema si jambo sahihi kiongozi kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya klabu na kuziingiza akaunti binafsi.
 Aveva na wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji ya Simba, juzi waliohiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) kwa tuhuma za kuchepusha fedha za mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi kutoka akaunti ya klabu hiyo na kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: