Na Afande Sele Theking
Hapo zamani za kale katika nchi ijulikanayo kwa jina la Tanzania iliyokuwa ikiongozwa na kiongozi mzalendo na jasiri aitwaye Kambarage Nyerere.
Alitokea mtu mmoja Tajiri mkubwa mweupe wa rangi mwenye kiburi, dharau na majivuno kwa wakaazi wa nchi ile na viongozi wake.
Katika huko kujikweza kwake siku moja mtu yule alikumbwa na tuhuma za kufanya makosa kinyume na taratibu za nchi ile ya Tanzania hivyo akatakiwa akamatwe kwa mujibu wa sheria kama wanavyokamatwa watu wengine wanaofanya makosa.
Basi yule mtu tajiri alipopata taarifa kwamba amevunja sheria za nchi, hivyo anapaswa kakamatwa alicheka tu na kujibu kwa kiburi na dharau kwamba katika nchi ile yeye haoni wa kumkamata kwani serekali yote kaitia 'mfukoni' mwake.
Khaaa...unajua nini kilichofuatia baada ya kauli ile ya dharau kumfikia yule mtawala mzalendo? .
Ule ndio ukawa mwisho wa yule tajiri fedhuli na baradhuli mkubwa kutumia kiburi cha fedha zake kuwadharau watanzania na taifa lao.
Alikiona 'cha mtema kuni' mzalendo Nyerere alifanya vile si kwa kumuonea yule mtu bali kwa kulinda heshima na utu wa watanzania,waafrika na watu weusi..
Historia hujirudia, zamu ya nani leoooo....Tanzania kwanza.
0 comments:
Post a Comment