BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HALIMA MDEE NA ESTHER BULAYA WAPATIKANA NA HATIA NA KUFUNGWA MWAKA MMOJA DODOMA


Dodoma. Halima Mdee na Esther Bulaya wamehukumiwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19.

Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo.

Mapema leo, Jumatatu Kamati ya Maadili ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.

Hata hivyo, Bunge liliendelea kujadili makosa ya wabunge hao wa Bunda na Kawe.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao. 


Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20/MWANANCHI

VIDEO YA HUKUMU
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment