BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AFISA WA CHEO CHA JUU TUME YA UCHAGUZI ALIYETOWEKA IJUMAA APATIKANA AKIWA AMEFARIKI DUNIA

Mwenyekiti wa IEBC nchini Kenya Wafula Chebukati.

Afisa wa cheo cha juu wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amepatikana akiwa amefariki.

Chris Musando ambaye ni meneja wa masuala ya teknolojia wa IEBC, alipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhi maiti mjini Nairobi

Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS na mmoja wa wafanyakazi wenzake.

Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.BBC
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment