RAIS John Magufuli amemuonya mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuacha kutetea masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kidini (Jumiki) Zanzibar.
Rais Magufuli hakumtaja Lowassa kwa jina wakati akionya wanasiasa wanaowatetea masheikh wa Uamsho, wanaokabiliwa na kesi ya uhaini mahakamani.
Hata hivyo, Lowassa anachunguzwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz kwa kuwatetea masheikh hao wakati wa hafla ya futari, jijini Dar es Salaam juma moja lililopita.
Akizungumza jijini jana wakati wa halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam utakaogharimu dola za Marekani milioni 421 (sawa na Sh. bilioni 926.2), Rais Magufuli alisema wanasiasa wanaotetea masheikh hao wanyamaze vinginevyo wataumia.
Aidha, Rais Magufuli alivitaka vyombo ya dola kuwakamata wale wote wanaotoa kauli za kutetea Uamsho ili wakaisaidie polisi katika uchunguzi bila ya kuangalia "anatembea taratibu, haraka, wala cheo alichonacho".
Kesi ya masheikh hao yenye mashtaka matatu, likiwamo la kuingiza watu nchini kushiriki vitendo vya ugaidi, kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inaendelea kwa mwaka wa nne sasa na Lowassa alimtaka Rais Magufuli kuwaachia huru.
Kuachia huru masheikh hao ilikuwa moja ya ahadi za Lowassa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambao Magufuli alishinda Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Wanaoropoka waisaidie polisi," alisema Rais Magufuli. "Polisi fanyeni kazi yenu, wajifunze kufunga mdogo wao... wataumia."
"(Na) wengine wanajitokeza hadharani kupinga. Watch out (chunga sana)."
Alisema kitendo cha serikali kuwashikilia masheikh hao kinamaanisha ina taarifa zote za kiuchunguzi hivyo mtu anapojitokeza kuwatetea ina maana aliwatuma au na yeye anahusika.
Masheikh wa Uamsho ambayo ni jumuiya ya Zanzibar walio mahabusu ni anayetajwa kuwa kiongozi Mselem Ali Mselem, Abdallah Said Ali, Farid Hadi Ahmed na Jamal Noordin Swalehe.
Wanadaiwa kusaidia kuwaingiza nchini Sadick Absaloum na Farah Omary ili kutenda makosa ya ugaidi.
BARUA KUMHITAJI
Rais Magufuli alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipinga hata masuala ya utaifa kama vile suala la madini kwa sababu wamepewa vijisenti.
Lowassa ambaye aliwania urais kwa tiketi ya Chadema na kushindwa, aliomba masheikh hao waachiliwe Juni 25 wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
Kwenye hafla hiyo Lowassa pia alisema ni jambo la fedheha kwa nchi illiyopata uhuru zaidi ya miaka 50 kuwaweka mahabusu viongozi wa dini bila kesi kusikilizwa mahakamani.
Kutokana na matamshi hayo, siku mbili baadaye DCI alimuandikia barua ya kumtaka afike makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam ambako alihojiwa kwa saa nne kisha kuachiwa kwa dhamana.
Alitakiwa kuripoti tena Alhamisi iliyopita, lakini aliporipoti Ofisi ya DCI ikampangia kufika hapo Julai 13 kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea.Nipashe MAGUFULI AMTOLEA UVIVU EDWARD LOWASSA KISA MASHEIKH WA UAMSHO
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment