BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MABAO 138 YATINGA NYAVUNI KTK MICHEZO 32 LIGI DARAJA LA KWANZA HATUA YA 9-BORA MOROGORO.

JUMLA ya bao 138 yamefungwa katika michezo 32 ya ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora huku klabu tatu za juu zikifanikiwa kutinga ligi kuu ya vocadom Tanzania bara kwa msimu wa mwaka 2012/2013 ambayo yatafikia tamati April 23 kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi hiyo klabu ambazo tayari zimefakiwa kucheza ligi kuu msimu ujao ni pamoja na Polisi Moro SC yenye pointi 17 ikiwa na mabao ya kufunga 14 na kufungwa manne, huku JKT Mgambo Shooting ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 15 ikifunga mabao 10 na kufungwa manne wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Tanzania Prinson yenye pointi 14 ambayo ina mabao 10 ya kufunga ikifungwa manne na kufanikiwa kwa klabu hizo kupata nafasi tatu za juu za ligi hiyo daraja la kwanza hatua ya tisa bora mwaka 2011/2012.

Katika mabao hayo ambayo yaliyaamua ushindi yalikuwa mabao 68 na mabao ambayo wapinzani walifungwa yalikuwa 70 na kufanya ligi hiyo kuwa na jumla ya idadi ya pointi kuwa 82 zilizokusanywa na klabu tisa ambazo zimeshiriki katika michezo 32 ya kuwania nafasi tatu za juu za kuingia ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.

Ligi hiyo daraja la kwanza msimu huu imeshuhudia Transit Camp ikiburuza mkia tangua ligi hiyo ianze na kufanyikiwa kupata pointi mbili kabla ya mchezo wa mwisho dhidi ya JKT Mlale leo ya kukamilisha ratibu majira ya saa 8 mchana huku Polisi Tabora ikichuana na Polisi Moro SC ikifanyika saa 10 jioni kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro wakati Tanzania Prinson itachuana na Polisi Dar saa 8 mchana huku Mbeya City FC ikicheza na JKT Mgambo Shooting majira ya saa 10 jioni kesho.

Katika msimamo huo unaonyesha kuwa jumla ya kadi 60 zimetolewa kwa wachezaji kutokana na adhabu mbalimbali zilizotolewa na waamuzi wa ligi hiyo kutokana na michezo hiyo 32 iliyofanyika kabla ya michezo ya mwisho.

Kadi hizo 60 ni kadi 56 za njano na kadi nyekundu zikitolewa nne kutokana na kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari huku kukiwa na wastani wa mabao mawili kufungwa kila mchezo mmoja huku kadi za njano zikiwa na wastani 2.33 kwa kila mchezo na kadi nyekundu wastani wa 0.13 kufanya idadi wa jumla wa kadi zote kufikia wastani wa 2.48 takwimu hizo kabla ya michezo ya mwisho ya ligi hiyo.

Polisi Dar imekusanya pointi 10 mabao ya kufunga 10 na kufungwa manne, Mbeya City FC pointi nane ikifumania nyavu kwa kufunga mabao saba na kufungwa nane, Rhino Rangers yenye ikiwa na pointi sita mabao ya kufunga manne na kufungwa manne, Polisi Tabora ikiwa na pointi tano ikifunga mabao saba na kufungwa mabao 13, JKT Mlale pointi tano mabao ya kufunga tano na kufungwa 13, Transit Camp ikiwa na pointi mbili ikiwa imefunga mabao mawili na kufungwa 12. 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: