Mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa jamii ya wafugaji mkoa wa Morogoro Seneto Parpai akifafanua jambo wakati wa mkutano uliolenga kutoa elimu ya namna ya kuchangia maoni ya marekebisho ya katiba mpya ili kutoa maoni mazuri wakati tume ya taifa ya kukusanya maoni ya marekebisho ya katiba hiyo katika maeneo mbalimbali ya vijijini juu ya kukusanya maoni hayo iliyofanyika katika
ukumbi wa Mount Uluguru mkoani hapa.
Msichana wa jamii ya wafugaji wa kimasai, Kelyana Kamunyu akichaangia mada katika mkutano huo.
Msichana, Tumaini Kochocho akieleza jambo wakati akichangia mada zilizokuwa zikijadiliwa.
Sarah Alakara, naye akifafanua jambo.
Mtoa mada katika mkutano huo, Pololetko Mgema akieleza jambo wakati akitoa mada ya maendeleo duni katika jamii na mchango wa elimu kwa jamii ya kifugaji.
Sehemu ya washiriki katika mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali.
SERIKALI imeshauriwa
kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika kutoa
maoni kabla ya tume ya taifa ya
kukusanya maoni ya marekebisho ya katiba mpya kufika katika maeneo mbalimbali ya
vijijini inayoendelea kukusanya maoni hapa nchini.
Akizungumza na wanafunzi
wa vyuo vikuu wa jamii ya wafugaji wa kimasai wanaoishi katika vijiji mbalimbali
vya mkoa wa Morogoro, Mwenyekiti wa Passad, Seneto Ole Parpai alisema kuwa ipo
haja kwa serikali kutoa elimu kwa wananchi wake hususani wa vijijini kabla ya
tume ya taifa kuwafikia ili kuweza kukusanya maoni yao juu ya muundo mpya wa katiba
mpya wanayotaka iwe.
Ole Parpai alisema kuwa ana
mashaka kwa tume ya taifa ya ukusanyaji wa maoni ya marekebisho ya katiba mpya kushindwa
kufanyakazi yake vizuri kutokana na wananchi wengi wanaoishi maeneo ya vijijini
kushindwa kujitokeza kwa wingi kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha wa kujitokeza
na kuchangia maoni yao amabyo nimuhimu katika uandikwaji wa katiba mpya.
“Mashaka yangu ni kuwa tume ya taifa ya
ukusanyaji maoni ya marekebisho ya katiba mpya kushindwa kupata wananchi pindi
watakapotembelea maeneo ya vijijini ili kutoa maoni yao juu ya marekebisho ya
katiba mpya” alisema Ole Parpai.
Ole Parpai alisema kuwa hali
hiyo ameiona wakati wa umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa jamii ya wafugaji
mkoa wa Morogoro ilipoandaa mikutano miwili katika vijiji vya wafugaji Wami-Sokoine
na Parakwiyo ili kuweza kutoa elimu kwa jamii hiyo waweze kutoa maoni pindi
tume ya taifa kukusanya maoni ya marekebisho ya katiba mpya itakapofika maeneo
hayo.
Alisema kuwa licha ya
vijana hao kuandaa mikutano miwili katika vijiji vya wami sokoine na Parokuyo
lakini wananchi wachache hususani wafugaji walijitokeza hivyo kuleta hali ya
wasiwasi na kutishia kutofanikiwa kwa tume ya ukusanyaji wa maoni kwaajili ya
kuandika katiba mpya ya nchi.
Aliongeza kuwa utolewaji
wa elimu hiyo itasaidia kuongeza wananchi kutambua umuhimu wa ushiriki wa
utoaji wa maoni amabo utaisaidia serikali katika kupanga utoaji wa huduma na
vipaumbele tofauti na sasa amabpo serikali inashindwa kupanga vipaumbele
kutokana na kutokuwa na idadi sahihi ya wananchi wake.
Alibainisha kuwa juhudi za
makusudi zinahitajika katika kuongeza weledi kwa wananchi hivyo kulifanya zoezi
hilo kufanikiwa kwa kiwango kikubwa na kuongeza maendeleo kwa wananchi kutokana
na serikali kufanikiwa kukidhi mahitaji ya raia wake.
0 comments:
Post a Comment