BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA POLISI MORO SC YATANGAZA KUKUMBWA NA UKATA WA KIFEDHA ZA KUENDESHEA TIMU LIGI DARAJA LA KWANZA.

Kikosi cha klabu ya Polisi Moro SC msimu wa 2016/2017 ligi daraja la kwanza Tanzania bara.

Juma Mtanda, Morogoro.
Licha ya klabu ya Polisi Morogoro Sport Club kufanya vizuri katika ligi daraja la kwanza, uongozi wa klabu hiyo imetangaza kukumbwa na ukata mkali wa fedha na kulazimika kusaka wafadhili wa kuinurusu kiuchumi.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Afisa Habari wa klabu hiyo, Clement Bazo alieleza kuwa timu ya Polisi Moro SC ni timu inayofanya vizuri katika ligi daraja la kwanza lakini kwa sasa klabu imekumbwa na ukata wa kifedha hali inayowapa wasiwasi kuihudumia kikamilifu.

Bazo ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo alisema kuwa ni kweli kabisa klabu yao ina ukata wa kifedha na kazi hali inayopelekea viongozi kukununa vichwa usiku na mchana kusaka wafadhili wa kuisaidia timu ili kuendeleza malengo yake ya kucheza ligi kuu msimu ujao.

“Hii timu ni moja ya timu hatari katika ligi daraja la kwanza, kwanza wachezaji wana uwezo wa kuifunga timu pinzani popote pale iwe uwanja wetu wa nyumbani au ugenini na unaweza kuona tuna pointi 12 katika michezo mitano.”alisema Bazo.

Akifafanua zaidi, Bazo alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika kulipa mishahara ya wachezaji, kugharamikia safari kwa michezo ya nje ya Morogoro na motisha kwa wachezaji.

“Kwa spidi hii ya wachezaji, kujituma na kucheza kwa bidii, kwa ajili ya timu, unaona kabisa wachezaji wana kitu wanatafuta na sio kingine bali kutimiza malengo yao ndani ya uwanja kuhakikisha timu inapata matokeo kila mchezo na hilo wameridhihilisha na wengi wao wana ndoto ya kucheza ligi kuu msimu ujao na hilo linawezekana.”alisema Bazo.

Kwa upande wa Kocha mkuu wa klabu hiyo, Ahmed Mumba alieleza kuwa kazi kubwa iliyopo mbele yao yeye na msaidizi wake, John Tamba ni kuwaandaa vijana kuhakikisha timu inaibuka na ushindi.

“Tuna mshukuru mwenyezi mungu, kati ya michezo mitano tuliyoicheza tumeshinda minne na kupoteza mmoja na kama benchi la ufundi inatuta morali wa hali ya juu kutoa ujuzi wetu na kuhamishia kwa wachezaji na wanafanyia kazi maelekezo yetu.”alisema Mumba.

Mumba alisema alieleza tayari timu imeanza maandalizi ya kuajindaa na michezo dhidi ya KMC FC ya Dar es Salaam katika uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani Oktoba 29 na Mbeya Warriors FC na malengo yao kupata pointi sita ili kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa vinara.

Wakati huo huo, timu ya Polisi Moro SC imeendeleza ubabe na kasi ya kukusanya polinti katika michezo ya ligi hiyo dhidi ya wapinzani wake baada ya jana kuisambaratisha Kurugenzi FC ya Mufindi kwa bao 2-1 katika mchezo mkali na kusisimua uliofanyika kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro.

Katika mchezo huo kiungo mshambuliaji, James Ambros alianza kuipatia Polisi Moro bao la kuongoza dakika ya saba baada ya kuitumia vyema krosi iliyomiminwa na mlinzi, Majid Musisi aliyepanda kusaidia mashambuliaji na kukwamisha mpira huo wavuni.

Baada ya kuingia kwa bao hilo kila timu ilicheza kwa tahadhari na kwenda mapumziki wenyeji wakiongoza kwa bao 1-0.

Mshambuliaji hatari na tegemeo wa maafande hao, Ramadhan Kapera alifunga bao la pili na ushindi dakika ya 52 kutokana na pasi ya, Fadhil Mzuma. 


Kurugenzi FC ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 89 lililofungwa na Miraji Mwilenga kwa mpira wa adhabu ndo nje ya 18 baada ya mlinzi wa Polisi Moro SC, Omari Mtaki kufanya madhabi na mwamuzi kutoka Arusha, Linus Joseph kuamuru adhabu hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: