ZINEDINE ZIDANE AJIUZULU UKOCHA MKUU KLABU YA REL MADRID
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ametangaza kujiuzulu nafasi nafasi hiyo leo Alhamisi ikiwa ni siku tano tangu aipe timu yake taji la ubingwa mara ya tatu mfululizo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Zidane anaondoka klabuni hapo kwa heshima baada ya kuitumikia kwa miaka miwili. Mfaransa huyo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo.
Kocha Zidane alithibithisha leo mchana kwamba ataachia nafasi hiyo kama kocha mkuu wa Real Madrid licha ya kuipataia mafanikio makubwa klabu hiyo.
Mkongwe huyo wa soka mwenye miaka 45, baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa ilikuwa inatabiriwa angeongezewa mkataba hadi mwaka 2020. Hata hivyo awali kulikuwa na presha kubwa kutoka uongozi wa Madrid kutokana na kutofanya vyema kwenye La Liga msimu huu ulioisha.
Makocha Arsene Wenger na Antonio Conte ni miongoni mwa wanaotajwa kumrithi Zidane, huku Conte akipewa nafasi kubwa Zaidi. Zidane alimrithi kocha Rafael Banitez Januari 2016 na msimu huo huo aliipa taji la Ligi ya Mabingwa timu hiyo.Mwananchi
0 comments:
Post a Comment