WAZIRI Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Kenya Raila
Odinga, amesema kuwa, serikali ya Kenya haitaruhusu machafuko na mauaji
ya kidini yakitokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 yarejee tena
nchini humo.
Raila amesema hayo alipokutana na
viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo mjini Mombasa na kuwahakikishia
kuwa machafuko ya mjini humo yatakoma mara moja.
Amesema Waislamu na
Wakristo kwa pamoja wanasisitizia haja ya kudumishwa usalama na amani
lakini wapo baadhi ya watu wasiolitakia mema taifa la Kenya ambao
wanaanzisha machafuko nchini humo.
Aidha Waziri Mkuu huyo wa Kenya
amelaani mauaji ya mwanaharakati wa Kiislamu Sheikh Aboud Rogo
yaliyofanyika Jumatatu wiki hii nchini humo na kuongeza kuwa, Kenya
haitoruhusu vita vya kidini vinavyosababishwa na maadui wa nchi hiyo
vitokee nchini humo.
0 comments:
Post a Comment