BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MABAO 15 YATINGA NYAVUNI KATIKA MICHEZO MINANE LIGI DARAJA LA KWANZA HATUA YA 9 BORA.



Mchezaji wa klabu ya Tanzania Prinson Henry Mwalugala kulia akitafuta mbinu ya kumtoka mlinzi wa Mbeya City Fideli Casto kushoto wakati wa ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora katika michezo inayoendelea kufanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. 

JUMLA ya mabao 15 yametinga nyavuni baada ya michezo minane ya ligi daraja la kwanza hatua ya tisa boara huku JKT Mgambo Shooting na Polisi Moro SC zikiwa zimejikusanyia pointi nne kila mmoja wakati wa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo inayoendelea kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

JKT Mgambo Shooting ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na mabao manne ya kufunga huku nyavu zake zikiwa zimeruhusu bao moja wakati Polisi Moro SC yenyewe ina mabao matatu ya kufunga na kufungwa bao moja baada ya kila timu kucheza michezo miwili.

Ligi hiyo jana ilikuwa katika mapumziko ya siku moja wakati inaendelea tena leo kwa mchezo wa Polisi Tabora dhidi ya Mlale JKT majira ya saa 8 mchana wakati mchezo wa pili utafanyika saa 10 kati ya Rhino Rangers na Transit Camp.

Mbeya City FC nayo ina pointi tatu na kufunga bao tatu na kufungwa mbili wakati Tanzania Prinson imekusanya pointi tatu na kufunga bao mbili huku nyavu zake zikiwa zimeruhusu bao mbili huku Polisi Tabora nayo ikiwa na pointi tatu na bao moja kutokana na kucheza mchezo mmoja.
Rhino Rangers imekusanya pointi mbili baada ya kutoa sare michezo miwili na kufunga bao mbili na kufungwa bao mbili wakati Polisi Dar imekuwa na pointi moja na kufunga bao moja na kufungwa bao moja huku JKT Mlale FC, Transit Camp ikiwa haina pointi kutokana na michezo miwili baada ya kupoteza mmoja na kutoa sare tasa ya bila ya kufungana.

Kutokana na michezo hiyo minane washambuliaji Mwagane Yeya wa Mbeya City FC na Fully Maganga wa JKT Mgambo Shooting wote wakiwa wamefumania nyavu kwa kupachika mabao wawili kila mmoja kutokana na michezo miwili.

Wakati klabu iliyofungwa mabao mengi katika michezo hiyo minane ni Transit Camp, JKT Mlale zote zikiwa zimeruhusu nyavu zao kutinga mabao matatu kila mmoja huku Mbeya City FC na JKT Mgambo Shooting ndizo zilizoshinda kwa idadi kubwa ya mabao kila mmoja akiwa amefunga mabao matatu wakati Tanzania Prinson na Polisi Moro SC wao wakiwa wameibuka na ushinda wa mabao mawili kwa kila timu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: