MIJI mbalimbali ya Tanzania imeshuhudia oparesheni kali ya inayoendeshwa
na polisi kwa lengo la kuwakamata watu wanaotatiza zoezi la kuwahesabu
watu linaloendelea Nchini kote.
Habari zaidi zinasema kuwa tayari watu kadhaa
wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kukataa kuhesabiwa.
Viongozi wa
Kiislamu wilayani Muheza wamehojiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama
Wilayani humo kwa tuhuma za kuwashawishi wananchi wasishiriki Sensa.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu alisema kuwa amewaita viongozi hao wa
dini kutokana na matamshi yao ya kuwahamasisha wananchi wasishiriki
Sensa.
MKOA WA KIGOMA:
polisi wamewakamata na kuwafungulia mashtaka watu
12 kwa kosa la kukataa kuhesabiwa.
Watu hao wamedai kuwa mila na desturi
zao haziruhusu binadamu kuhesabiwa kama wanyama.
Sensa ya watu na
makazi iliyoanza Agosti 26, imekumbwa na changamoto nyingi huku Waislamu
wakitakiwa kulisusia zoezi hilo baada ya serikali kukataa kuorodhesha
suali la dini katika madodosa ya sense hiyo.
Sensa ya mwaka 2002
ilionyesha kuwa idadi ya Watanzania ilikuwa takriban milioni 34.5 na
inatarajiwa kwamba idadi ya watu kwenye sense ya mwaka huu itakuwa zaidi ya watanzania hao.
0 comments:
Post a Comment