BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAANDISHI WA HABARI WAADHIMISHA MAADHIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI 2017 KWA MBWEMBWE MTUPU MOROGORO

Sehemu ya waandishi wa habari mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye maandamo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyoanzia eneo la Shan kisha mzunguko wa magari wa SUA, Masika hadi Savoy ambako kulifanyika kongamano la kujadi mambo mbalimbali yanayogusa tasnia hiyo.PICHA ZOTE NA MTANDA BLOG
Sifuni Mshana wa ITV Morogoro hapa kama anaongoza maandamano hayo lakini sio

 Hawa nao wakiwa wamebeba bango la Abood Medi
Mwandishi na Mtangazaji wa michezo kituo cha redio na luninga Clouds media Morogoro, Peter Andrew akiwa amebeba bango lenye ujumbe wa kuwataka polisi kuwalinda waandishi wa habari katika majukumu yao katika maandamano hayo

Kundi la waandishi wa habari na watangazaji wa kituo cha redio cha SUA FM katika maandamano hayo
Baadhi ya viongozi akiwemo mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari Morogoro (MSJ) Nongwe S. Nongwe (mwenye koti), Amina Juma Gazeti la Mwananchi Morogoro (aliyeshika Mwamvuli), Ashton Balaigwa kwenye kofia na Loveness Batuki wakiwa katika maandamano hayo.
Mkuu wa mkoa mstaafu wa Morogoro, Steven Mashishanga na Mratibu wa Morogoro Press Club, Thadei Hafigwa wakicha wakati wa kupokea maandamano ya waandishi katika kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Savoy
Meneja wa shirika la nyumba la taifa mkoa wa Morogoro (NHC) Veneranda Seiff akizungumza jambo huku mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe kushoto na mkuu wa mkoa mstaafu wa Morogoro, Steven Mashishanga wakifuatilia maelezo yake.
Waandishi wakifuatia jambo
Katibu Msaidizi wa Morogoro Press Club, Jimmy Mengele akisoma lisara juu ya changamoto zinazoikumba club huyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe (hayupo pichani)
Mwenyekiti wa Morogoro Presss Club, Nikson Mkilanya akizungumza jambo kwenye kongamano hilo.
Sehemu ya waandishi wa picha kwa ajili ya luninga na magazeti wakichukua habari wakati matukio yakiendelea kwenye meza kuu katika kilele cha maadhimisho hayo.
Mwandishi wa ITV Morogoro, Sifuni Mshana akiwa na kijana Frank Kaundula katika ukumbi huo.
Baadhi ya waandishi wa kituo cha redio cha SUA FM na Mweka Hazina wa Morogoro Press Club, Merina Robert wa kwanza kushoto wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
Waandishi wa gazeti la Mtanzania mkoa wa Morogoro, Lilian Justice kushoto na Ashura Kazinja wakiwa kwenye kongamano hilo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kupokea maandamano yaliyoanzia Shan kuelekea mzunguko wa magari wa SUA kisha Masika na kumalizikia Savoy ambako kulikuwa na kongamano la kujadili mambo mbalimbali yanayohusu tasnia ya habari katika kilele hicho kinachoadhimishwa kila mwaka Mei 3.
Hapa ni baadha ya waandishi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
Mwandishi mkongwe wa kituo cha redio cha SUA, Gerald Lomile akifuatilia matukio katika kongomano hilo.
Kassim Lyimo wa TV Imaan (mwenye koti) na Rashid Abdallah Mtagaluka wa kituo ca redio cha MUM FM wakiwa miongoni wa waandishi waliohudhuria kongamano hilo.
Mratibu wa Morogoro Press Club, Thadei Hafigwa, Afisa habari halmashauri ya Mvomero, Juma kamia na mwenzake wa ofisi ya mkuu wa mkoa Chimesela wakifuatia matukio katika kongamano hilo
Baadhi ya timu ya waandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd wakiongozwa na bosi wao, Amina Juma kulia, Habiba Yahya na Hamida Sharifff wakiwa kwenye kongamano hilo.

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI BILA MASLAHI BORA KWA WAANDISHI WA HABARI INAWEZEKANA?
Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari ndo imepita, japokuwa siku hii naiona kama ni maadhimidhi ya siku ya Wamiliki wa Vyombo vya habari wanaotaka vyombo vyao viwe na Uhuru wa kuandika habari bila 'mipaka'.

Kwa kuwa dhana nzima ya maadhimisho ilitwishwa kwa waandishi, tumeshuhudia Waandishi wa habari kuwa ndio waliobeba msalaba wa kuwasilisha madai na mada mbalimbali kuhusu kudai uhuru huo wa vyombo vya habari wakati wa maadhimisho ya siku hiyo jana.

Sijui ni kwa sababu sikuona na kusikia tukio hilo Live kutoka jijini Mwanza, katika mada na hotuba zote ikiwemo ya Waziri mwenye dhamana ya habari, sikusikia kikitajwa kwa dhati na uzito wake kilio cha umuhimu wa kuwalazimisha wamiliki wa vyombo vya habari kuboresha maslahi ya waandishi wa habari ikiwemo mazingira bora ya kazi, mikataba ya kazi na kulipwa mishahara kwa wakati!

Bila shaka waandishi wa habari mnajua, ukiacha vyombo vya habari vya serikali, walimiki karibu wote wa vyombo binafsi kiukweli hawazingatii kikamilifu maslahi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wengine katika vyombo vyao.

Imeshakuwa ni kama jambo la kawaida kuwakuta waandishi wa habari wengi tu, wapo kazini kusaka habari lakini hawajalipwa mishahara kwa uhakika kwa miezi au miaka kadhaa, na hata akiamua kuacha kazi hapati pensheni zake kwa kuwa mwajiri hajapeleka makato ya pensheni hizo kwa miaka kedekede!

Wamiliki hawa hawatoi maslahi bora kwa waandishi na watumishi wao wengine kutokana na sababu mbalimbali, lakini binafsi nahisi ni kutosimamia vyema vyombo hivyo hasa upande wa menejimeti kwa kuwa vyombo hivi kama taasisi yoyote vinapaswa kuwa na menejimenti imara, zenye viongozi wenye uthubutu na weledi wa hali ya juu katika kuratibu na kusimamia wafanyakazi kimaslahi na kiutendaji, na pia wenye malengo na mikakati thabiti ya kibiashara badala ya kuwa na viongozi kina boraliende!

Hivyo basi hali hii ya maslahi duni inawafanya waandishi wa habari wa vyombo vingi hapa Tanzania ambao wengi wanao weledi wa kutosha kutaaluma, kutoweza kuutumia vizuri Uhuru wa kuandika habari hata uhuru huo ukiwepo kwa zaidi ya asilimia mia moja.

Hii ni kwa kuwa mazingira hayo ya kutopatiwa maslahi huwageuza bila hiari waandishi hao kuwa mateka wa watu wa mitaani wanaowalipa fedha ili kuandikiwa habari zinazolinda maslahi yao hasa wanasiasa pengine hata wsuza dawa za kulevya!

Katika mazingira hayo usitarajie kuona habari za kijamii na za kutetea na kulinda maslahi ya wanyonge na za kutetea na kulinda utaifa zikiripotiwa kwa kina na mwandishi wa kada hiyo.

Na kwa kweli katika mazingira ya njaa hakuna mwandishi kutoka vyombo visivyotoa maslahi ambaye anaweza kukwepa au kunusurika kutekwa. Maana adui wa kwanza duniani ni njaa, hata mwanajeshi shupavu aliyejificha handakini akitwangwa na njaa sawasawa anatoka nje.

Kwa hiyo, ikiwa waandishi wanataka kuwa salama na kuendana na weledi katika kazi yao hii adhimu, kwa kuwa jana walijifunga kibwebwe katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya uhuru wa vyombo vya habari, Sasa nashauri bila kulazimisha Wajipange kwa umoja wao watenge pia SIKU YA MASLAHI YA WAANDISHI WA HABARI.

Maana katika hali ya mazingira ya hali ya sasa, nionavyo mimi hata uhuru wa vyombo vya habari ungekuwa mkubwa kiasi gani mwandishi asiyepewa maslahi bora na Chombo husika bado uhuru huo hautakuwa na tija inayotarajiwa kwake.

Wakatabahu
BN 0789498008
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment